Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 30Article 560482

Habari za Biashara of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Njombe kuwa kitovu cha uzalishaji wa parachichi Tanzania

Njombe kuwa kitovu cha uzalishaji wa zao la parachichi nchini Njombe kuwa kitovu cha uzalishaji wa zao la parachichi nchini

Mkoa wa Njombe, umelengwa kuwa kitovu kikuu cha uzalishaji wa zao la parachichi baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali uliowavutia wakulima wengi kutoka sehemu tofauti nchini.

Haya yamebainishwa na Meneja Maendeleo wa Chama cha Kilimo Tanzania (TAHA), Anthony Chamanga wakati akitoa mafunzo kwa wakulima 120 kutoka mikoa ya Arusha, Mbeya, Iringa wa zao hilo mkoani humo.

Amesema kuwa Mkoa huo una rutuba nzuri inayoruhusu ukuaji wa zao hilo na kufafanua kuwa kawaida mti mmoja wa parachichi unaweza kutoa hadi kilo 150 za matunda hayo endapo wakulima watafuata taratibu za kupanda zao hilo.

Zao la parachichi linahitaji maji mengi ili kuweza kutoa matunda mengi ya kutosha, na ni moja kilimo chenye faida kubwa kwani tunda hili linatumika katika shughuli nyingi za uchumi.