Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 19Article 572653

Habari za Biashara of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

RC Mtaka awataka wajasriamali wa zabibu kuongeza ubunifu

RC Mtaka awataka wajasriamali wa zabibu kuongeza ubunifu RC Mtaka awataka wajasriamali wa zabibu kuongeza ubunifu

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka wajasiriamali, wasindikaji wa viwanda vya kutengenea mvinyo kupanua wigo wa soko ili kujitosa katika masoko ya Afrika Mashariki na yale ya SADC.


Amesema kuwa sekta ya uzalishaji wa mvinyo huo kwa mkoa wa Dodoma una nafasi kubwa ya kuimarika zaidi endapo wazalishai hao wataongeza ubunifu kwa kutumia nafasi zilizotolewa na Serikali za kuwekeza kwenye kilimo cha zabibu.

Kwa dhana hiyo, amewataka wajasiriamali wa viwanda vya mvinyo, wasindikaji na wafungaji bidhaa sio tu kuja na bidhaa bora na zenye viwango, lakini pia wafikirie fursa zilizopo katika masoko ya Afrika Mashariki na SADC.