Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 27Article 554086

Habari za Biashara of Friday, 27 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Rais Samia ametoa Tsh. Milioni 600 mnadani Pugu

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesikiliza kero za wafanyabiashara wa mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam ukiwemo utaratibu wa ulipaji ushuru kuwa, biashara katika mnada huo inaanza saa moja asubuhi, lakini changamoto wanayoipata ni suala la ukatishaji wa ushuru ambapo watumishi wanafungua ofisi saa tatu asubuhi kwa mujibu wa mwongozo wa minada.

Akifafanua juu ya utatuzi wa kero hiyo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaelekeza watendaji wa mifugo wa wizara hiyo, kurekebisha mwongozo wa mnada ili kuruhusu shughuli za huduma kuanza saa moja asubuhi badala ya saa tatu asubuhi.

“Lengo la ziara hii ni kuangalia utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua ujenzi wa uzio unaozunguka mnada huu pamoja na kupokea na kushughulikia kero zinazowakabili wafanyabiashara.” Amesema Ulega.

Ameongeza kuwa mwongozo huo uliwekwa wa saa tatu asubuhi kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanaweza kufanya ujanja wa kwenda na mifugo katika minada kisha kuondoka nayo kwa kisingizio cha kukosa wateja na kuikosesha serikali mapato.

Pia Naibu Waziri Ulega amewaarifu wafanyabiashara hao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupa mnada wa Pugu Shilingi Milioni 600, kwa ajili kutengeneza eneo la kunyweshea mifugo maji na mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kazi hiyo itakayoanza wiki ijayo.