Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 09Article 556474

Habari za Biashara of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

SIDO yapewa baraka kutengeneza vifungashio mafuta ya kula Kigoma

Wizara ya viwanda na SIDO vya tengeneza vifungashio vya mafuta ya mawese Wizara ya viwanda na SIDO vya tengeneza vifungashio vya mafuta ya mawese

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema shirika la kuhudumia viwanda vidogo mkoa wa Kigoma SIDO limeshatengeneza sampuli za vifungashio vya mafuta ya Mawese vitakavyotumiwa na wakulima kwa sasa.

Waziri huyo amesema kwa kuanzia SIDO imetengeneza sampuli ya vifungashio hivyo kuanzia vya lita tano na lita ishirini na vifungashio hivyo viko katika mfumo wa ndoo za chuma.

Aidha Waziri huyo amebainisha kuwa, hatua hiyo ni moja kati ya utekelezaji uliopangwa wa kuhakikisha kuwa wanatengeza mazigira rafiki kwa wajasiriamali wa mafuta hayo ili kuweza kushindana kimataifa.

Hata hivyo hapo awali, Wizara kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa cha biashara cha ITC waliweza kuiwesha SIDO kutengeza mashine zinazoweza kukamua mafuta hayo kwa muda wa masaa mawili tu kutoka masaa nane hapo awali.