Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 17Article 552046

Habari za Biashara of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Samia azitaka Taasisi za Fedha kurefusha muda wa ulipaji madeni.

Rais Samia akiwa na viongozi kwenye mkutano wa SADC Rais Samia akiwa na viongozi kwenye mkutano wa SADC

Rais Samia Suluhu Hassani leo Agosti 17, 2021 wakati akifungua mkutano wa 41 wa SADC wa wakuu wa nchi wa Serikali wa jumuiya ya mandeleo kusini mwa Afrika SADC pamoja na kujitambulisha rasmi kwa wakuu wa nchi na serikali ya jumuiya hiyo ameziomba nchi zinazoendelea na taasisi za kifedha za Kimataifa kutoa misamaha na kurefusha muda wa ulipaji wa madeni wa nchi zinzoendelea mpaka janga la Ugonjwa wa UVIKO 19 litakapokwisha.

Hii inatokana na Dunia kuporomoka kiuchumi na kuathirika kwa safari za nje ya nchi kutokana na maeneo mengi kufungwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Kutokuwa na muingiliaono wa watu kwa Mataifa wanachama SADC na mdororo wa biashara kumepelea uchumi kushuka kwa kiasi kikubwa na taifa kama Tanzania kukumbwa na mfumko wa bei.