Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 06Article 561646

Habari za Biashara of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kurekebisha usimamizi wa NARCO

Serikali kurekebisha usimamizi wa NARCO Serikali kurekebisha usimamizi wa NARCO

Serikali imeamua kurekebisha mfumo wa usimamizi wa Kampuni ya taifa Mifugo (NARCO), ikiwa ni juhudi za pamoja za kuboresha utendaji wa sekta hiyo nchini.

Haya yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa NARCO, Prof Peter Msoffe, na kusema kuwa mabadiliko yaliyofanyika yamepelekea shirika hilo kugawanyika katika kurugenzi kuu mbili.

Amesema kuwa kurugenzi ya kwanza itahusika na masuala yote ya uzalishaji, maendeleo ya miundombinu na utendaji kazi wa shirika hilo.

"Kurugenzi hii ya kwanza itakuwa na sekta kuu tatu, sekta ya kwanza ni Uzalishaji, miundombinu, ya pili ni usimamizi na udhibiti wa magonjwa ya wanyama na ya tatu itahusika na malisho ya wanyama" Amesema Prof Msoffe.

Kurugenzi ya pili itahusika na huduma za kampuni, na itagawanyika katika sekta kuu mbili, ambazo amezitaja kuwa ni rasilimali watu na utawala, na sekta ya pili itahusuka na mipango, usimamizi na tathimini.

Ameongeza kusema kuwa mabadiliko haya yataboresha idara zote muhimu katika kampuni hiyo kama vile, kitengo cha usimamizi na manunuzi, ICT na Takwimu, usimamizi wa fedha huduma za ndani, idara ya mahusiano kwa Umma (PR) pamoja na biashara.