Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 17Article 572053

Habari za Biashara of Wednesday, 17 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali kuzishika sekta binafsi maendeleo ya viwanda

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo

mikakati itakayozipa nafasi kushiriki katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini sambamba na kutambua maeneo yanayovutia na yasiyovutia kwa uwekezaji wa sekta binafsi.

Kauli hii imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo wakati akijibu swali la mdau katika Kongamano la miaka 60 ya Uhuru leo Novemba 17, 2021 lililotaka kufahamu kuhusu muelekeo wa sekta ya viwanda na biashara nchini.

Aidha ameongeza kusema kuwa Serikali inatambua kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo ni muhimu kiuchumi japo hayavutii kuwekeza na kuwa kwa mantiki hiyo inachukua jukumu la kuwekeza moja kwa moja katika maeneo hayo kama vile vile kwenye viwanda vya sukari.

Amesema kuwa Serikali inaendelea na kuhimiza ujenzi wa mitaa ya viwanda ili kuongeza juhudi za kufikia uchumi wa bluu.