Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 19Article 552517

Habari za Biashara of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Serikali njiani kurasimisha soko la ndizi kimataifa

Zao la Ndizi kupata soko nje Zao la Ndizi kupata soko nje

Serikali ya Tanzania inalenga kuongeza uzalishaji wa zao la ndizi ili kukidhi mahitaji makubwa ya masoko ya nje na ndani.

Waziri wa Kilimo Adolf Mkenda ameyasema hayo alipotembelea Kamati ya Bunge ya kilimo, Ufugaji na Maji. Amesema ameweka mikakati kukamilisha uzalishaji wa zao la ndizi ili kufikia soko la kimataifa na kukidhi mahitaji biashara ya ndizi.

"Mpango wa kufungua fursa zao la ndizi upo njiani, hii yote ni katika kukidhi mahitaji muhimu ya nyumbani na kuuza nje" amesema Mkenda.

Waziri amewahakikishia wabunge kuleta watalaamu wenye uzoefu wa kukuza viwanda vya kilimo, kutokana na uzalishaji mkubwa wa ndizi ambao umeonekana kufanywa zaidi na Tanzania na Uganda kwa upande wa Afrika Mashariki.

Waziri ameitaka kamati kukutana na wadau wa zao la Ndizi, wataalamu wa mazao, watafiti ,watalaamu wa masoko na kampuni za kuuza mazao nje ya nchi ili kufikia lengo.