Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 11Article 562618

Habari za Biashara of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yaahidi kuongeza uzalishaji Kagera Sugar

Serikali yaahidi kuongeza uzalishaji Kagera Sugar Serikali yaahidi kuongeza uzalishaji Kagera Sugar

Waziri Mhagama, amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imepanga kuongeza uwekezaji nchini kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi.

Amesema kuwa kazi ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na fursa za kutosha pamoja mazingira rafiki yatakayo wezesha utekelezwaji wa fursa hizo ili kuwavuta wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza nchini.

Ametoa kauli hii wakati alipotembelea kiwanda cha uzalishaji sukari cha Kagera ili kuangalia uwekezaji uliofanywa katika kiwanda hicho kwa kufuata sheria za kazi pamoja na uchangiaji wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii NSSF.

Kwa kuzingatia malengo hayo ya kuinua uwekezaji nchini, Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kiwanda hicho kinaongeza uzalishaji ili kuteka soko la sukari ndani na nje ya nchi.