Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 10Article 556786

Habari za Biashara of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yatoa bilioni 50 kununua mahindi

Serikali yatoa bilion 50 kununua mahindi Serikali yatoa bilion 50 kununua mahindi

Serikali imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kununua mahindi kutoka kwa Wakulima wa maeneo mbalimbali nchini.

Haya yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiahirisha mkutano wa nne wa Bunge leo Agosti 10 ,2021 jijini Dodoma na kuongeza kuwa ununuzi huo unatarajiwa kuanza jumatatu ya Septemba 13, 2021.

Waziri Mkuu, amesema fedha hizo zitatolewa kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), ambao umekuwa ukifanya kazi hiyo ya kununua mahindi ya Wakulima. Aidha, Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha baada ya kusikia kilio cha Wakulima wa maeneo mblimbali nchini kuwa mahindi yao yamekosa soko.

Bunge limeahirishwa hadi tarehe 2 Novemba mwaka huu.