Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 14Article 542596

Habari za Biashara of Monday, 14 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Serikali yatoa miezi 3 uendeshaji nyama, maziwa

Serikali yatoa miezi 3 uendeshaji nyama, maziwa Serikali yatoa miezi 3 uendeshaji nyama, maziwa

Alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokutana na Bodi ya Maziwa na Nyama kwa ajili ya kutoa maelekezo mbalimbali.

Ulega alisema mpaka sasa serikali inatumia pesa nyingi kila mwaka kuagiza maziwa nje ya nchi na kwamba endapo kungekuwa kumewekwa mazingira mazuri ya uzalishaji wa maziwa hayo nchini, badala ya fedha hiyo kutumika kuagiza bidhaa hiyo nje ingetumika kuboresha uzalishaji wa maziwa ya ndani.

“Maziwa mengi yanapotea huko kwa wafugaji, lakini moja ya sababu kubwa ya maziwa hayo kupotea ni kutokana na kutokuwapo kwa mipango mizuri ya namna ya kuyakusanya au kuyapata, kwa sababu vibebeo vyenyewe vya maziwa hayo ni gharama kubwa kwa hiyo wengi wao wanashindwa kumudu kuvinunua,” alisema Ulega.

“Sasa nakuagizeni, changamkeni. Tunataka vibebeo vya maziwa vienee huko kwa wazalishaji na mshirikiane na watu wa sekta binafsi, wenye viwanda vidogo na vikubwa kusambaza hizo, sambazeni vifaa vya kubebea maziwa kwa vikundi vya kinamama na vijana na mpite kwenye hizi halmashauri zenye mifugo,” alisema Ulega.

“Tunataka hivi vikundi vya wafugaji vya kinamama na vijana watumie pesa zile za halmashauri za asilimia 10 wanazopewa wakusanye maziwa yaliyopo kule vijijini ili yachakatwe, kwa hiyo kitengo cha masoko mnatakiwa kuamka na kuleta matokeo makubwa.”

Alisema serikali inatumia Sh. bilioni 14 kila mwaka kuagiza maziwa nje, na endapo kutakuwa na mipango mizuri, badala ya kiasi hicho cha fedha kutumika kuagiza bidha hiyo nje ya nchi, itatumika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ndani ya upatikanaji wa maziwa kwa wingi.

Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk. George Msalya, alisema uzalishaji wa maziwa nchini umeongezeka kutoka lita bilioni 3.1 mwaka 2019/2020 hadi lita bilioni 3.4 mwaka 2020/2021.

Pia alisema usindikaji wa maziwa hayo umeongezeka kutoka lita 203,600 kwa siku mwaka 2019/2020 hadi kufikia lita 208,000 kila siku mwaka 2020/2021.