Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 30Article 554338

Habari za Biashara of Monday, 30 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Sifa za mtambo wa kukausha nguzo uliozinduliwa SAO HILL

Mtambo wa kwanza kukausha Nguzo  Afrika Mashariki wazinduliwa Tanzania Mtambo wa kwanza kukausha Nguzo Afrika Mashariki wazinduliwa Tanzania

Mtambo wa kwanza wa kisasa wa kukausha nguzo katika nchi za Afrika Mashariki na Kati umezinduliwa katika kiwanda cha nguzo cha Sao Hill kilichopo wilayani Mufindi.

Mtambo huo umezinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Sao Hill, Godlisten Minja amesema kuwa maamuzi ya kufunga mtambo kwenye kiwanda hicho yamefanyika ili kuongeza ubora wa nguzo na kuongeza uzalishaji.

Hizi ni sifa za mtambo huo.

1. Mtambo huo unakausha nguzo kati ya siku nne hadi 12 kutegemea hali ya ubichi tofauti na kutumia jua kukausha nguzo hizo ambapo nguzo hukaushwa kwa takriban miezi mitatu hadi minne.

2. Nguzo 800 hadi 900 zinakaushwa kwa wakati mmoja kutegemeana na ukubwa wa nguzo.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amepongeza Sao Hill kwa kufunga mtambo huo wa kisasa ambao haukuwepo hapa nchini na kufanya upanuzi wa uzalishaji wa nguzo katika kiwanda hicho.

Amewahakikishia wazalishaji hao na wengine uhakika wa soko la nguzo hizo kwani kazi ya usambazaji umeme mijini na vijijini inaendelea. Aliwataka pia kuongeza uzalishaji wa nguzo hizo.

Amesema kuwa Serikali inategemea kuwa bei ya nguzo hizo zitapungua kutokana na kuongezeka kwa viwanda vya nguzo ambavyo kwa sasa ni zaidi ya 11 .