Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 20Article 558502

Habari za Biashara of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Soko la sukari ya Zanzibar bado ni kitendawili Bara

Soko la sukari ya zanzibar bado ni kitendawili Bara Soko la sukari ya zanzibar bado ni kitendawili Bara

Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda visiwani Zanzibar, Omar Said Shaaban, amefafanua mzozo wa uuzwaji wa sukari inayozalishwa visiwani humo kutouzwa sehemu nyingine hasa Tanzania bara.

Amefafanua kwa kusema kuwa, Mzozo huo umekuwa moja kero za Muungano, na kuwa suala hili limejadiliwa katika kikao cha kutatua kero za Muungano huku likibaki bila kupata utatuzi hadi hivi sasa.

Aidha Waziri huyo, ametoa maoni kuhusu suala hili kwa kueleza kuwa suala la uwekezaji katika taifa, ni suala huria, lakini kama taifa ni lazima kumuhakikishia muwekezaji uhakikka wa soko hivyo kitendo cha sukari hiyo kutouzwa bara kinakwamisha juhudi za mapinduzi ya viwanda visiwani humo.

Ameongeza kusema kuwa, hoja zilizotolewa na upande wa bara, zinadai kuwa kutoruhusu sukari ya zanzibar kuuzwa bara ni hatua za kuvilinda viwanda vya ndani, na kuwa sukari hiyo haitoshelezi soko la ndani la Zanzibar.

"Mnapozungumza viwanda vya ndani mnaionaje Zanzibar? je Zanzibar sio sehemu ya viwanda vya ndani? Waziri Omar