Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 10Article 556777

Habari za Biashara of Friday, 10 September 2021

Chanzo: Habarileo

TCCIA yasaini makubaliano kutatua kero kwa wafanya biashara

Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA) Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA)

Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA) limeingia makubaliano ya ushirikiano na taasisi tatu kwa lengo kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sekta ya uchimbaji na gesi asilia na kuondoa changamoto mbalimbali kwa wafanyabiashara.

TCCIA imesaini mkataba huo wa ushirikiano baina yake yake na Jumuiya ya Watoa Huduma wa Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS), Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda wa Zanzibar(ZNCCIA) na Saccos ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE).

Akizungumza katika hala ya utiaji saini wa makubaliano yao jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa, Rais wa TCCIA Paul Koyi amesema kupitia ushirikiano huo wafanyabiashara, wenye viwanda sambamba na wanachama wote wa taasisi zilizohusika watapiga hatua ya kimaendeleo kwani baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili zitaweza kutatuliwa kwa urahisi.

“Tumekuwa tukishirikiana katika mambo mbalimbali kabla ya kuingia kwa makubaliano haya, imani yetu kuanzia sasa nguvu itaongezeka na hivyo kutuwezesha kutatua kwa haraka changamoto mbalimbali tukiwa wa moja wenye lengo moja la kuleta maendeleo katika taifa,” alisema Koyi.

Akizungumzia ushirikiano wa TCCIA na ZNCCIA, Koyi alisema makubaliano hayo yaliyosainiwa leo yatasaidia kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania Bara na Visiwani huku ushirikiano wake na TASWE ukilenga kuwasaidia wanachama wa taasisi hiyo utatuzi wa kero wanazokutana nazo hususani wanapofanya biashara na wadau kutoka mataifa ya nje.

Naye mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi nchini (ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim alisema kupitia ushirikiano huo, wanaamini kuwa elimu kuhusu fursa zinazopatikana katika bomba la mafuta, zitaweza kuwafikia wananchi

Mwanzilishi wa TASWE, Anna Matinde alisema matarajio ya wanachama wa taasisi anayoiongoza watakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yao hasa pale wanapokutana na maswali kutoka kwa wateja wao wa mataifa mengine juu ya bidhaa zao.