Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 18Article 552121

Habari za Biashara of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

TOP 10: Kampuni 10 zenye mitaji mikubwa kibiashara Afrika Mashariki

TOP 10: Kampuni 10 zenye mitaji mikubwa kibiashara Afrika Mashariki TOP 10: Kampuni 10 zenye mitaji mikubwa kibiashara Afrika Mashariki

Kampuni nne kutoka Tanzania zimetajwa kwenye orodha ya makampuni yenye mitaji mikubwa zaidi sokoni kwa nchi za Afrika Mashariki. Kampuni hizo ni pamoja na Tanzania Breweries Limited (TBL), Vodacom tawi la Tanzania, Tanzania Cigarette Company (TCC) na National Microfinance Bank (NMB).

Kwa mujibu wa jarida la African Business, Kampuni ya huduma za mawasiliano Safaricom ya Kenya imeongoza kwa kumiliki mtaji wa dola za Marekani Bilioni 13.3 ikifuatiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) yenye mtaji wa dola za Marekani bilioni 1.4.

Hii hap ani orodha ya makampuni 10 yaliyotajwa kuwa na mitaji mikubwa zaidi kwenye soko la Afrika Mashariki.

1. Safaricom - Kenya $13.3bn 2. TBL - Tanzania $1.4bn 3. Equity - Kenya $1.3bn 4. KCB - Kenya $1.2bn 5. EABL - Kenya $1.1bn 6. Vodacom - Tanzania $744m 7. TCC - Tanzania $733m 8. Co-op Bank - Kenya $708m 9. NMB - Tanzania $505m 10. Stanchart - Kenya $490m