Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 26Article 553834

Habari za Biashara of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

TPC: "Wafanybiashara acheni kupandisha bei ya sukari"

TPC: TPC: "Wafanybiashara acheni kupandisha bei ya sukari"

Menejimenti ya kiwanda cha sukari cha TPC Ltd wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, imesema hakuna upungufu wa sukari kwa sababu kuna ziada ya zaidi ya tani 18,873 ya bidhaa hiyo.

kauli hiyo inakuja baada ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa ya sukari katika mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara, Singida na Kilimanjaro.

Ofisa Mtendaji Utawala wa kiwanda hicho, Jafary Ally amesema “Ghala la kiwandani lina uwezo wa kuhifadhi tani 7,000, tulizonazo hadi leo asubuhi ni tani 3,375, ghala la Kahe lina tani 14,873, ghala la kampuni ya Setway tani 615 na bado uzalishaji unaendelea,”.

Alisema kwa siku kiwanda hicho kinazalisha tani 600 za sukari, huku mauzo kwa siku moja ni tani 450 jambo ambalo linaonesha kuendelea kuwapo kwa akiba ya bidhaa hiyo.

“Mkoa wa Kilimanjaro pekee unahitaji tani 60 za sukari kwa siku moja, ukijumlisha kwa pamoja na mikoa ya Manyara, Arusha ni mahitaji ya tani 270, bado uwezo wetu uko juu,” amesema.

Mtanda amesema serikali inafuatilia baadhi ya wafanyabiashara ili kubaini wanaopandisha bei ya bidhaa hiyo.

Amesema serikali imejiridhisha kuwa hakuna upungufu wa sukari mkoani Kilimanjaro na akatoa mwito kwa wananchi watoe taarifa wakibaini wafanyabiashara wanaoficha bidhaa hiyo.