Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 04 28Article 535738

Habari za Biashara of Wednesday, 28 April 2021

Chanzo: eatv.tv

TRA yaanza kutoa Elimu mlango kwa mlango

TRA yaanza kutoa Elimu mlango kwa mlango TRA yaanza kutoa Elimu mlango kwa mlango

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kwamba katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kutokuwa kero kwa walipa kodi ili kuongeza mapato imeanza kutoa Elimu ya mlipa kodi mlango kwa mlango lengo ni kuwa karibu na walipa kodi-

Submitted by Martha Magawa on Jumanne , 27th Apr , 2021 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo.

ili kutatua changamoto zinazojitokeza.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo wakati akizungumza na EATV ambapo amesema kuwa kwa sasa wanahakikisha wanaondoa changamoto na kero zilizokuwa zikiwakuta walipa kodi nchini kama ambavyo aliagiza Rais katika maagizo yake kwa Mamlaka hiyo.

"Tunatoa Elimu kwa mlipa kodi mlango kwa mlango na tumeanza katika mikoa ya kikodi Temeke, Ilala na Kilimanjaro lengo likiwa ni kuwa karibu na walipa kodi ili watueleze changamoto wanazokutana nazo", amesema Kayombo.

Aidha ameitaja mikoa ambayo tayari imeanza zoezi la mlango kwa mlango kuwa ni mikoa ya kikodi Temeke, Ilala, na Kilimanjaro ambapo lengo ni kuwaweka karibu zaidi walipa kodi.

 

Join our Newsletter