Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 23Article 553207

Habari za Biashara of Monday, 23 August 2021

Chanzo: Mwananchi

Taarifa ya TCRA kuhusu kupungua kwa miamala ya simu

Taarifa ya TCRA kuhusu kupungua kwa miamala ya simu Taarifa ya TCRA kuhusu kupungua kwa miamala ya simu

Imeelezwa kuwa tangu kuanzishwa kwa tozo ya miamala ya simu Julai 15 mwaka huu, idadi ya miamala imepungua.

Agosti 21, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) amesema miamala milioni 9.9 ni wastani wa miamala kwa siku moja, hivyo kwa siku 28 miamala iliyofanyika ni zaidi ya milioni 277.2.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa TCRA, Jabir Bakari amesema upungufu huo ni mdogo kama alivyoeleza Waziri Mwigulu ikilinganishwa na takwimu za kipindi cha nyuma.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Watanzania wameendelea kutumia huduma za miamala kama kawaida na kwa kipindi cha wiki nne tangu kuanzishwa kwa tozo hizo Serikali ikikusanya Sh48.48 bilioni.

“Katika wiki nne za mwanzo jumla ya miamala milioni 9.9 ilifanyika, haina tofauti sana na siku za nyuma ilipokuwa milioni 10 na milioni 11, tofauti sio kubwa,” alisema Dk Mwigulu, bila kueleza mlinganisho wa thamani ya miamala katika kipindi hicho na kilichopita.

Kwa mujibu wa takwimu za mawasiliano za robo mwaka za TCRA, Julai 2020 jumla ya miamala milioni 288.35 yenye thamani ya Sh11.3 trilioni ilifanyika.

Kwa Agosti peke yake jumla ya miamala iliyofanyika ilikuwa 288.56 yenye thamani ya Sh11.07 trilioni na Septemba miamala ilikuwa 299.25 ya Sh11.55 trilioni.

Takwimu za mawasiliano zilizotolewa hivi karibuni na TCRA mpaka Juni, 2021 watumiaji wa huduma za simu nchini walikuwa 53,182,651.

Kuhusu hatima ya tozo hizo, Nchemba alisema suala la mapitio ya tozo za simu kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu ndani ya kipindi kifupi, taarifa yake itatolewa kwa kuwa kuna kipengele kimoja kilitakiwa kufanyiwa kazi zaidi na tayari imekamilika na ipo kwa Waziri Mkuu.