Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 23Article 553090

Habari za Biashara of Monday, 23 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Tani 5,551 za Parachichi za Tsh. Bilioni 19 zimeuzwa nje

Soko la parachichi lazidi kushamiri Tanzania. Soko la parachichi lazidi kushamiri Tanzania.

Zao la Parachichi ambalo linapatikana katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania limeonekana kuzalishwa kwa wingi na kuwaokomboa watanzania kutoka kwenye wimbi la umasikini, kuimarisisha familia kiuchumia pamoja na lishe.

Mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe,Tanga, Kilimanjaro, Kigoma, Kagera , Katavi na morogoro ni mikoa maarufu kwa uuzaji na uzalishaji wa zao la parachichi.

Taaarifa iliyotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa NBS imesema Tani 19,449 za parachichi ziliuzwa na kuzalishwa mwaka 2016/2017.

Wakati huo huo Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) katika taarifa yake iliyotolewa mwaka 2018 inaonesha tani 5,551 zenye thamani ya dola 8.5 ziliuzwa barani Ulaya, Africa na Asia.

Vyanzo mbali mbali vya takwimu za kibiashara zinaonesha mauzo ya parachichi nje ya nchi kwa mwaka 2019 yaliongezeka ukilinganisha na mwaka 2013. Hivyo zao la parachichi limeonekana kuongezeka mwaka kwa mwaka na kuleta faida kwa taifa na wakulima.

Hali hiyo imeendelea kuimarisha soko la parachichi la Tanzania kutoka asilimia 0.1 hadi 0.4 kwa kusaidiwa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) licha ya changamoto ya UVIKO-19

Kampuni inayosimamia zao la parachichi ya Rungwe huzalisha jumla ya Tani 5000 kutoka kwa wakulima wadogo.