Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 14Article 557317

Habari za Biashara of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tanzania kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza ya utalii Afrika Mashariki

Tanzania kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza ya utalii Afrika Mashariki Tanzania kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza ya utalii Afrika Mashariki

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya kwanza ya Utalii ya Ukanda wa Afrika Mashariki (EARTE) 2021, Oktoba 9, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Makao Makuu ya EAC, Maonesho haya ya utalii yatafanyika katika mzunguko wa watalii wa Kaskazini mwa Arusha kuanzia Oktoba 9, hadi Oktoba 16.

Tamasha la EARTE 2021, linafanyika kwa mara ya kwanza limetajwa kuwa litakua ni la kipekee katika katika ukanda huu, na lengo kubwa ni kuvitangaza na kukuza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuandaa onesho la utalii kwa ukanda wa EAC, ambapo siku tatu za kwanza zimetengwa kwa maonesho na siku nne kufanya safari za kutembelea na kujifunza kuhusu maeneo mbalimbali ya utalii kwenye maeneo makubwa ya vivutio ya Bara na Zanzibar.

Maonesho hayo yatafanyika kwa mzunguko kati ya nchi wanachama wa EAC, na kaulimbiu ya mwaka huu imeitwa, "kukuza utalii wenye ustahimilivu kwa maendeleo ya umoja wa kijamii na uchumi".

Mnamo Julai, mawaziri wa EAC wanaosimamia idara za wanyamapori na utalii waliidhinisha Mkakati wa Uuzaji wa Utalii wa EAC kwa kipindi cha 2021-2025.

Mkakati huo unazingatia kuanzishwa kwa maonesho ya utalii kama jukwaa linalowaleta watendaji wa utalii wa serikali na zisizo za serikali katika kuonesha vivutio vingi vya utalii na anuwai na fursa za uwekezaji katika ukanda huu..