Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 11 18Article 572287

Habari za Biashara of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tanzania na Burundi kuipa nguvu sekta ya posta

Tanzania na Burundi kuipa nguvu sekta ya posta Tanzania na Burundi kuipa nguvu sekta ya posta

SHIRIKA la Posta Tanzania limepokea ujio wa Postamasta Mkuu wa Burundi Madame Lea Ngabire aliyeambatana na ujumbe wake ambapo lengo la ujio wao nchini ni kubadilishana uzoefu ili kuendelea kuwahudumia wananchi.

Kaimu Posta Mastamkuu Macrice Mbodo amesema ugeni wa Posta Burundi Postamasta Mkuu ni ujio wenye faraja kwa Tanzania hasa ikizingatia mahusiano mema yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, si kuwa ni rafiki bali ni ndugu.

"Kama mnavyofahamu hivi karibuni Rais wa Burundi Evariste Ndaishimiye alitembelea Tanzania kwa ushirikiano katika ngazi ya kitaifa na yapo mengi yaliyokubalika kufanywa na nchi zetu, leo na sisi Posta tumefuata nyayo za viongozi wetu wakuu ndiyo maana unaona Posta ya Burundi na uongozi mzito upo hapa kwetu leo kwa ziara ya kikazi na kujifunza.

"Kama mtakumbuka Tanzania ilishiriki Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja wa Posta Duniani uliofanyika mwezi Agosti, 2021 kule Abidjan, Ivory Coast. Tanzania ilipata mafanikio makubwa na kunadika historia ya kuaminiwa na kuchaguliwa katika mabaraza makuu muhimu ya uongozi kwenye Umoja wa Posta Duniani,"amesema Mbodo

Ameongeza kwamba Tanzania ilishinda na kuwa Mjumbe wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani( Council of Administration) na pia ilifanikiwa kushinda kiti cha Baraza la Uendeshaji (Postal Operations Council) la Umoja huo.

Amesema sambamba na hilo Tanzania iliaminiwa kuongoza Kamati ya Pili ya Huduma za Posta na Biashara Mtandao(Physical Services and E-Commerce) ikiwa ni mwenyekiti mwenza pamoja na Uswis (Nchi inayoongoza kwa ubora wa huduma duniani).

Pia shuguli mbalimbali zilizofanyika wakati wa Mkutano huo Mkuu wa 27 wa Posta duniani , Shirika la Posta Tanzania lilifanikiwa kufanya mazungumzo ya ushirikiano wa kibiashra na kubadilishana uzoefu na Posta mbalimbali duniani.

"Lengo likiwa ni kujifunza yale mema ambayo wengine wameyafanya na sisi tuyafanye kwa faida ya wananchi wetu, ikizingatiwa Shirika hili ni mali ya Serikali kwa asilimia 100, hivyo ni mali ya watanzania. Jambo hili limezaa matunda mnayoyaona leo.

"Tulipokutana Abidjani tulizungumza na kukubaliana kushirikiana na kubadilishana uzoefu na wenzatu wa Burundi na ugeni huu mkubwa wa kutoka nchi ya Burundi ukiongozwa na Postamasta Mkuu Lea Ngabire na wasaidizi wake hawa wawili ni matunda ya mazungumzo yetu,"amesema Mbodo

Ameongeza ugeni huo umekujakwa lengo la kujifunza na kuchukua yale mema ambayo sisi tumeyafanya, wamefurahi. Na hakika wameona yale tunayofanya katika kuifanya Posta yetu kuwa ya kidijitali na pia kuona huduma zinazotolewa kwenye ofisi za Posta kwa niaba ya Serikali.

Amefafanua kama mnavyofahamu Tanzania ni mwenyeji wa Umoja wa Posta za Afrika (pale mjini Arusha) ,nasi Shirika la Posta tumedhamilia kutoa uwakilishi sawia na heshima tuliyopewa, leo Mmeona Burundi wamekuja hapa kujifunza, lakini kabla ya mwaka huu kwisha mtawaona Kenya nao watakuja na wengine mwakani.

"Huu ndiyo mwelekeo wetu na tungependa wananchi wayajue haya na waendee kutuunga mkono tunapotekeleza Azma ya kiongozi wetu wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ,ambaye anaifungua nchi kimataifa ili kuleta uwekezaji wa kiuchumi kwa ustawi wa watanzania.

" Sitawasemea lakini mtawasikia na wao watasema walichokiona katika sehemu za utendaji walizozitembelea maana walikuwa na ziara ya maeneo ya kazi leo kwa ofisi ya Dar es salaam. Hii ni heshima kubwa sana kwetu na hatuna budi kueleza haya kwa umma wa watanzania ili waweze kuunga mkono juhudi zinazofanywa , na pia ni haki yao kupata taarifa hizi muhimu kwa kuwa ni Shirika lao,"amesema Mbodo.