Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 09Article 562231

Habari za Biashara of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: eatv.tv

Tanzania yakumbushia nchi wahisani kukamilisha ahadi zao

Tanzania yakumbushia nchi wahisani kukamilisha ahadi zao Tanzania yakumbushia nchi wahisani kukamilisha ahadi zao

Tanzania imezikumbusha nchi zilizoendelea kutekeleza kikamilifu ahadi ya kutoa fedha kwa Bara la Afrika kwa lengo la  kusaidia kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabianchi jambo litakaloziwezesha nchi hizo kutumia rasilimali kidogo ilizonazo katika kupambana na janga la UVIKO-19.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, katika mkutano wa Kimataifa wa Amani unaofanyika Roma, Italia na kufafanua kuwa katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Mazingira uliofanyika mwaka 2015 jijini Paris, Ufaransa, nchi zilizoendelea ziliazimia kutoa kiasi cha dola bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea kusaidia kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabia nchi ahadi ambayo mpaka sasa haijatekelezwa.

Katika mkutano huo Tanzania imeendelea kupaza sauti kuhusu kuzingatia usawa katika upatikanaji na usambazaji wa chanjo ya UVIKO – 19 hususani katika Bara la Afrika ili kuleta usawa,haki na uwajibikaji katika kupambana na ugonjwa huo.