Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 19Article 552394

Habari za Biashara of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tanzania yavuna bil 43/- biashara ya vitunguu EAC

Tanzania yavuna bil 43/- vitunguu EAC Tanzania yavuna bil 43/- vitunguu EAC

TANZANIA imeingiza sh bilioni 42 .5 mwaka jana kwa kuuza tani 42,000 za vitunguu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi Kilele inayojishughulisha na masuala ya maua, mboga, matunda, vyakula vya mimea inayotokana na mizizi na viungo (TAHA), Simon Mlai alisema hayo wakati wa kuzinduliwa kwa Kongani ya Vitunguu inayoundwa na Umoja wa Wakulima wa Vitunguu Arusha.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Kata ya Ilikiding'a , Halmashauri ya Arusha, Mlai alisema kongani hiyo itawezesha wakulima kunufaika na mikopo, masoko na mitaji.

Alisema Taha itaendelea na juhudi za kuunganisha wakulima hao ili waone tija katika uuzaji wa zao hilo la kitunguu sanjari na kunufaika na mitaji pamoja na kupata uhakika wa upatikanaji wa pembejeo muhimu kwaajili ya wakulima kunufaika na kilimo hicho nchini

Mlai alisema muungano wa wakulima utawezesha TAHA kutoa elimu na kuwaachia wakulima kuitumia hatimaye kunufaika na mnyororo wa fursa za masoko zilizopo EAC na kwenye nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Mwakilishi wa Shirika la Trias, Julius Mlambo aliwapongeza wakulima wa vitunguu kwa kuwa na umoja na kwamba safar ndo kwanza imeanza.

Mkulima kutoka kata ya Sambasha, Julius Ole Laizer alishukuru uwepo wa kongani hiyo itayokusaidia wakulima kujadili changamoto za bei na masoko ya vitunguu.

"Tunaomba hili suala la rumbesa liangaliwe kwa umakini badala ya kuuza gunia mbili za vitunguu unajikuta unauza gunia moja na unapata hasara sababu madalali ni wengi tena wanakuja mashambani sasa umoja huu utatusaidia kuuza bidhaa zetu nje ya nchi kwa uhakika haswa nchi za EAC"alisema Ole Laizer.