Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 24Article 553342

Habari za Biashara of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Thamani ya manunuzi migodini yafikia Dola Milioni 579.

Thamani ya manunuzi migodini yafikia Dola Milioni 579. Thamani ya manunuzi migodini yafikia Dola Milioni 579.

Imeelezwa kuwa yapo Mafanikio Makubwa yaliyotokana na Ushiriki wa Watanzania katika Utoaji wa Huduma Migodini huku thamani ya manunuzi yaliyofanyika ndani ya nchi yakipanda hadi kufikia Dola Milioni 579.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula wakati akizungumza na Waandishi wa Habari

Pamoja na kuwepo kwa mafanikio hayo, imeleezwa kuwa, bado ipo haja kwa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuhakikisha inaifungamanisha ipasavyo Sekta hiyo na uanzishwaji wa viwanda vinavyozalisha malighafi kwa ajili ya kuhudumia migodi nchini.

‘’Ushiriki wa watanzania kwenye utoaji wa huduma umezidi kupanda siku hadi siku, tulikuwa tunapata takwimu hapa leo, thamani ya manunuzi ya ndani kwenye migodi mikubwa imefikia karibu Dola milioni 500 na kitu, hili ni jambo kubwa sana,’’ amesema Kitandula.

Aidha, Kitandula ametumia fursa hiyo kuzipongeza benki za ndani kwa kuanza kutoa mikopo kwa wachimbaji ikiwemo miradi mikubwa katika Sekta ya Madini na kuzitaka kuangalia namna zinavyoweza kushirikiana na benki za nje ili kuwawezesha wawekezaji katika Sekta ya madini kupata mikopo itakayowezesha kuanzishwa kwa miradi mikubwa.