Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 08Article 556276

Habari za Biashara of Wednesday, 8 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tsh. Bilioni 281.7 zimekopeshwa kwa wakulima kupitia TADB

Tsh. Bilioni 281.7 zimekopeshwa kwa wakulima kupitia TADB Tsh. Bilioni 281.7 zimekopeshwa kwa wakulima kupitia TADB

HADI Julai 31,2021 Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imekwishatoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 281.74 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kilimo, ufugaji na uvuvi nchini.

Hayo yamesemwa Bungeni mjini Dodoma leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Yusufu Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini Almas Maige (CCM).

Maige alitaka kujua, ni wakulima wangapi wadogo wadogo wamepata mikopo kutoka Benki ya Kilimo ili kukuza tija kwa wakulima wadogo.

Pia aliuliza, riba za Benki ya Kilimo zinatofauti gani na riba za benki za biashara ili kumsaidia mkulima mdogo.

Maaauni alisema mikopo hiyo iliyotolewa na benki hiyo imewanufaisha wakulima 1,514,695 vikiwemo vyama vya wakulima 151 hapa nchini.

Sambamba na utoaji wa mikopo ya moja kwa moja, benki ya maendeleo ya kilimo inasimamia Mfumo wa Dhamana kwa Wakulima wadogo ( SCGS) unaolenga kuchagiza mabenki na taasisi za fedha kuongeza ukopeshaji katika sekta ya kilimo.

Hadi kufikia mwisho mw Juni 2021, SCGS ilitoa udhamini wa mikopo kwa

wakulima Wadogo 11,244, vikundi vya wakulima 181 na SMEs 43 waliopata mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 89.92 kutoka benki tisa washiriki katika uendeshaji wa mfuko wa SCGS.