Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 16Article 551782

Habari za Biashara of Monday, 16 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Uagizaji mafuta na gesi wapaa kwa 12.9%

Faida ya uingizaji wa mafuta na gesi Faida ya uingizaji wa mafuta na gesi

Waagizaji wa gesi na mafuta ya Petrol (LPG) wametakiwa kujipongeza na uagizaji huo baada ya serikali kuimarisha na kukuza soko hilo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Takwimu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) zimeonyesha uagizaji wa mafuta na gesi umekuwa kwa asilimia 12.9% kutoka Tani 107,083 mwaka 2016/2017 hadi Tani 120,961 kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Pia imekuwa kwa asilimia 20% kwa mwaka uliofuata na kufikia tani 145,800 na kuongezeka kwa asilimia 30% hadi kufikia Tani 190,248 kwa mwaka wa fedha 2019/20

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Bwan. Godfrey Chibulunje amesema, Hii inaonesha kwamba kuna ukuaji endelevu wa nishati ya Petrol na Gesi sokoni, kutokana na mabadiriko ya jamii kutoka kwenye njia za kitamaduni za kupikia hadi kwenye kutumia gesi.

" Ongezeko hili kubwa la kuingiza gesi nchini ni matokeo ya mamlaka ya Ewura kwa kufanya kampeni na kuongeza uelewa juu ya matumizi ya gesi" alisema Chibulunje.

Kwa Upande wake Mkuu wa Biashara na Usambazaji wa gesi ya Oryx nchini Bwan. Mohamed Mohamed Tanzania alisema ukuaji huo unatia moyo na Oryx itaendelea kuwekeza katika hilo.

"Tuna kila sababu ya kuendelea kuwekeza kutokana na unapatikanaji wa fursa zilizopo kwenye mapato na uwekezaji mzuri uliopo Tanzania" Alisema Bwn. Mohamed.

Aliongeza kuwa, kuna ukuaji mkubwa wa uwekezaji kwenye suala la mafuta na gesi kwa kuangalia miundombinu, vituo vya kuagiza, ujenzi wa depo mpya za mafuta na kukua kwa mtandao wa usambazaji.