Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 19Article 558298

Habari za Biashara of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: ippmedia.com

WMA yatakiwa kuthibiti wadanganyifu wa vipimo

WMA yatakiwa kuthibiti wadanganyifu wa vipimo WMA yatakiwa kuthibiti wadanganyifu wa vipimo

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ametoa wito kwa watumishi wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kufanya kazi kwa bidii na uadilifu katika kumlinda mwananchi dhidi ya udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Kigahe ameyasema hayo leo  alipotembelea Ofisi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini na pia kupata fursa ya kutembelea ofisi za Wakala za Mikoa ya Temeke, Kinondoni, Ilala, ofisi ya vipimo vya bandarini vilivyopo SIDO vingunguti na baadaye kutembelea na kukagua kituo cha upimaji cha Misugusugu kilichopo Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na watumishi, Kigahe amesema kuwa wafanyabiashara wa jumla na rejareja wamekuwa wadanganyifu kwa kuwa wakinunua bidhaa viwandani wanapunguza ujazo wake halisi.

“Kumekuwa na tabia ya wanyabiashara kupunguza ujazo halisi wa bidhaa kwa lengo la kujipatia faida kubwa, nimejionea leo mifuko ya misumari iliyokamatwa na Wakala wa vipimo ambapo misumari hiyo ilikuwa imefungashwa katika kilo 50 lakini walipopima walikuta kilo 45" amesema Kigahe.