Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 02 22Article 525802

Business News of Monday, 22 February 2021

Chanzo: HabariLeo

Wachimbaji wa dhahabu waingiza Bil 2.9/-

Wachimbaji wa dhahabu waingiza Bil 2.9/-

JUMLA ya Sh bilioni 2 .9 zimekusanywa kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Januari 2021 kupitia sekta ya madini mkoani Simiyu.

Hayo yalisemwa na Ofisa Madini Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, Joseph Kumburu kwenye mkutano na wachimbaji wadogo mkoani humo uliofanyika Kata ya Dutwa wilayani Bariadi mkoani hapa.

"Mfano mwezi huu haujaisha lakini tumeshakusanya Shilingi milioni 430 kwa hiyo mwezi ukiisha tutakuwa na zaidi ya Shilingi bilioni tatu, tumejiwekea makisio ya kila mwezi kukusanya Shilingi milioni 600 hadi 700, tunakaribiana na Shinyanga," alisema.

Mwenyekiti Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Simiyu (SIMIREMA), Paul Matendele alisema wao ndio mwenye kushughulikia changamoto za wachimbaji hao kwa mujibu wa miongozo ya serikali.

Aidha alisema kuwa baadhi ya wachimbaji wa madini wamekuwa wanachangia migogoro kwa kutokuheshimu chama cha wachimbaji wa madini kwa kudhani kipo tu na kusahau kuwa kipo kwa mujibu wa sheria za nchi kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali ya wachimbaji wa madini.

Join our Newsletter