Uko hapa: NyumbaniBiashara2022 01 10Article 584554

Habari za Biashara of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wadau waiomba Serikali kushusha bei mashine za ETS

Wadau waiomba Serikali kushusha bei mashine za ETS Wadau waiomba Serikali kushusha bei mashine za ETS

Wafanyabiashara wenye viwanda nchini wameiomba Serikali ipunguze gharama za stempu za kielektroniki (ETS). Ombi hilo linakuja huku Kamati ya Maboresho ya Sera za Kodi inayohusika na matayarisho ya Bajeti IRA.

Serikali ikikaribisha wadau kutoa maoni yao kuhusu bajeti ya mwaka 2022/2023. Kamati hiyo itaanza kazi yake Februari 2022 hadi Februari 10 na itapokea maoni ya wadau, kufanya uchambuzi na majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusu sera za kodi na usimamizi wake.

Akielezea matamanio yao katika mwaka mpya wa fedha ujao, Mtaalamu wa Sera wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Frank Dafa alisema kuwa ETS inaongeza gharama za kufanya biashara hivyo jambo hilo linapaswa kutazamwa upya.

"Tunafikiri sasa Serikali italian-galia upya hill suala la ETS. Hata kama sio kuondoa utaratibu huo, basi kupunguza gharama zake kwa sababu zilizopo sasa zinakwaza biashara," alisema.

Dafa aliitaka Serikali kuweka ulinzi wa kikodi kwa viwanda vya ndani na kutoza kodi kubwa kwa bidhaa za nje.