Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 13Article 557191

Habari za Biashara of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wafanyabiashara wakubwa wameilipa TRA Tsh. Trilioni 1.02 kwa miezi miwili.

Wafanyabiashara wakubwa wameilipa TRA Tsh. Trilioni 1.02 kwa miezi miwili. Wafanyabiashara wakubwa wameilipa TRA Tsh. Trilioni 1.02 kwa miezi miwili.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kiasi cha shilingi Trilioni 1.02 kwa mwezi July na August kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa huku ikiwa na matumaini ya kutimiza lengo la makusanyo ya mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na walipa kodi wakubwa kutoka kwenye sekta mbalimbali za uzalishaji nchini ikiwemo taasisi za fedha, kampuni za mawasiliano, ujenzi, bima na nyinginezo.

Kidata amezipongeza taasisi zinazolilipa kodi kwa hiari bila kusukumwa na kueleza kuwa jambo hilo ndio sababu ya Mamlaka hiyo kufikisha kiasi cha Trilioni 1 ndani ya miezi miwili ya mwanzo tangu kuanza kwa mwaka mpya wa fedha.

TRA imesema kuwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 walifanikiwa kukusanya jumla ya Tsh. Trilioni 18.06 huku walipa kodi wakubwa wakichangia kiasi cha shilingi Trilioni 6.5 ambayo ni asilimia 38 ya mapato yote. Mwaka huu wa fedha 2021/2022 TRA wanatarajia kukusanya Tsh. Trilioni 22 huku shilingi Trilioni 9 zikitarajiwa kutoka kwa walipa kodi wakubwa.