Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 05 03Article 536203

Habari za Biashara of Monday, 3 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wakulima kahawa wapata faida zaidi

Wakulima kahawa wapata faida zaidi Wakulima kahawa wapata faida zaidi

Programu hiyo inalenga kuongeza tija kwenye uzalishaji, ubora wa mazao pamoja na kuwaunganisha wakulima hao na masoko.

Uboreshaji wa zao hilo unafanywa na Programu ya AGRI-CONNECT ambayo inalenga kuboresha mnyororo wa thamani wa zao hilo chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Akizungumza kwenye mkutano huo, kiongozi wa timu ya watekelezaji wa Programu hiyo, Colin Scott, alisema inalenga kuboresha maeneo sita ya mnyororo wa thamani wa zao la kahawa.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na kusaidia kuboresha sera na mazingira ya biashara ya zao hilo, kuongeza tija kwenye uzalishaji na usindikaji uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini ili kuwaunganisha wakulima na masoko, maghala, viwanda na kurahisisha usafirishaji wapembejeo za kilimo.

Vilevile, Scott alisema programu hiyo inalenga kusaidia kuongezeka kwa uwekezaji hasa wa sekta binafsi kwenye mnyororo wa thamani wa zao hilo, kuongeza ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kusaidia kuhamasisha lishe bora.

“Programu hii, mbali na kutekelezwa katika mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini, inatekelezwa Zanzibar na katika maeneo haya yote programu inatarajia kuwafikia wakulima wadogo 150,000,” alisema Scott.

Alisema programu pia imejikita kuboresha mnyororo wa thamani wa chai na mazao ya bustani.

Vile vile, alisema programu hiyo inanatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu na wadau wa sekta binafsi.

Alisema mkutano huo pia ulilenga kujadiliana namna ya kuondoa mwingiliano wa shughuli miongoni mwa wadau wanaoshiriki kuwasaidia wakulima ili kuepuka kuwachanganya wakulima hasa taasisi hizo zinapofanya kazi zinazofanana.

Akielezea ufadhili Umoja wa Ulaya katika mnyororo wa thamani wa zao la kahawa mwakilishi wa Jumuiya hiyo, Andrea Massarelli, alisema Tanzania ina fursa nyingi kwenye sekta ya kilimo.

Alisema Tanzania ina ardhi ya kutosha inayoweza kusaidia kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwamo kahawa na ndio sababu ya Jumuiya hiyo kufadhili.

 “Jumuiya ya Umoja wa Ulaya imejikita katika kusaidia uongezaji wa tija na ufanisi wa sekta ya kilimo hasa kwenye zao la kahawa,” alisema Massarelli.

Baadhi ya wadau wa mnyororo wa thamani wa kahawa walisema ubora wa kahawa inayozalishwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini umeanza kuongezeka na hivyo kuwa na uhakika wa soko lenye faida.

Mmoja wa wadau hao, Sandra Ca’rdenas, mwakilishi wa Taasisi ya usambazaji wa teknolojia za kisasa za usindikaji wa kahawa inayojulikana kama Msumbi Afrika JM ESTRADA kutoka Colombia, alisema ili kuongeza ubora zaidi wakulima wanatakiwa kutumia mitambo ya kisasa ya kusindika kahawa.

Wadau wenginge waliowasilisha mada kwenye mkutano huo ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Taasisi ya Mitaji ya Kilimo Biashara (Bamboo Agribusiness Capital) ya nchini Kenya pamoja na mashirika ya Solidaridad na Vi-Agroforestry yanayotekeleza miradi chini ya programu ya AGRI-CONNECT.

Kahawa ni miongoni mwa mazao ya biashara ambayo yanaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni, lakini katika miaka ya karibuni uzalishaji ulianza kushuka hasa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokana na sababu mbalimbali.

Join our Newsletter