Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 10 09Article 562261

Habari za Biashara of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wakulima wa Korosho wakubali bei kikomo ya 2,445

Wakulima wa Korosho wakubali bei kikomo ya 2,445 Wakulima wa Korosho wakubali bei kikomo ya 2,445

MNADA wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2021-2021,umefanyika jana Mkoani Mtwara kwa wakulima wa zao hilo kutoka wilaya ya Newala na Tandahimba kukubali kuuza  korosho zao tani 1486 kwa bei ya juu ya shilingi 2445 na bei ya chini shilingi 2231 kwa kilo moja ya korosho daraja la kwanza ghafi.

Katika mnada huo uliofanyika katika wilaya ya Newala chini ya Chama kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala(TANECU),na kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, jumla ya makampuni 16 yalijitokeza yakiwa na bei tofauti tofauti,ambapo Wakulima hao wamesema Mnada umeanza kwa bei nzuri hivyo hawaoni sababu ya kuacha kuuza korosho zao.

Makampuni yaliyofanikiwa kufika katika bei kikomo ya mnada huo huku tani walizonunua pamoja na bei yake zikiwa kwenye mabano ni A.M.J (tan 500 bei 2231), Dizygotec (tani 300 bei 2445);Alpha Namata (tani 250 bei 2235);P.H agro (tan 200 bei 2325);Lyon (tani 50 bei 2400).

Makampuni yaliyoshindwa kufikia bei kikomo katika mnada huo huku bei na tani walizohitaji kununua zikiwa kwenye mabano ni pamoja, Element limited( tani 500 bei 1800);. Pompus (tani 1486 bei 1859); Sibatanza (tani 1486 bei 2200);Pecommunities (tani 100 bei 2300); Beaform tani( 50 bei 1600) na Alpha Namata tena  (tani 200 bei 2200).

Makampuni mengine Mohammed inter (tani 300 bei 1880);Senaco (tani 200 bei 1767);Afrisha (tani 50 bei 1572); Export trade(tani 300 bei 2225) Vanency (tan 200 bei 2105).

Akihutubia kabla ya kuanza mnada huo Brigedia Jenerali Gaguti aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika kuacha tabia ya kuwarubuni wakulima na kueleza  atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Alisema viongozi wa vyama vya ushirika wanatakiwa kutenda haki katika ununuzi wa zao la korosho kwa ajili ya  kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao.

"Nawasihi wakulima kuendelea kutunza korosho zenu katika mazingira mazuri ili zinapoletwa sokoni ziweze kuwa na ubora na hivyo kuwavutia wanunuzi."alisema GagutiMnada wa pili wa korosho kutoka Chama Kikuu cha Ushirika cha Tanecu unatarajia kufanyika Oktoba 15 mwaka huu katika wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.