Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 08 18Article 552247

Habari za Biashara of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Watalii wengine 200 wawasili nchini

Watalii kutoka Israel wawasili Nchini Watalii kutoka Israel wawasili Nchini

Kundi la mwisho la watalii mia mbili (200) kati ya Watalii 550 kutoka nchini Israel waliokuja kutembelea vivutio katika hifadhi za taifa za kanda ya kaskazini na visiwa vya Zanzibar limewasili huku kundi la pili la watalii mia mbili (200) likiondoka kurejea nchini kwao.

Kundi hili la tatu la watalii linakamilisha idadi ya watalii 550 waliokuwa wanatarajiwa kuwasili nchini kwa mwezi Agust ambao nao watakuwa nchini kwa takriban siku saba kutembelea hifadhi za Serengeti na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro watalii hao wamelakiwa na mkurugenzi wa idara ya mashariki ya kati wizara ya mambo ya nchi za nje balozi Hemed Mgaza na maafisa wa bodi ya utalii nchini.

Baadhi ya watalii wanaotarajia kuondoka baada ya kumaliza utalii wao wameeleza kufurahishwa na vivutio vya kipekee walivyo viona.