Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 06 11Article 542242

Habari za Biashara of Friday, 11 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wavuvi watangaziwa neema vifaa, vyombo

Wavuvi watangaziwa neema vifaa, vyombo Wavuvi watangaziwa neema vifaa, vyombo

Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Abdalla Hussein Kombo, aliyasema hayo huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Dimani, Mwanaasha Khamis Kombo.

Mwanaasha alitaka kujua iwapo serikali ina mpango wa kuwasaidia wananchi hao ili kuongeza kipato na kunufaika na uchumi wa bluu.

Waziri Kombo alisema mpango huo utafanyika kupitia utaratibu wa benki na kwamba wananchi watapata fursa ya kupata mikopo itakayowasaidia kuwekeza katika uvuvi.

Aidha, alisema mpango huo utakuwa ukifanyika pale serikali itakapopata fursa ya miradi ya maendeleo yenye kulenga huduma kama hiyo.

Alisema wizara itashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutafuta njia endelevu na mbadala za kuwasaidia wavuvi boti na vifaa kwa ajili ya shughuli zao.

Hata hivyo, alisema kuwapo kwa mfuko maalumu wa kuwasaidia wavuvi katika shughuli zao ni njia mojawapo ya kuwawezesha wavuvi hao kupata fedha za kuwekeza katika uvuvi.

Aidha, alieleza kwamba kwa sasa wanawashajihisha wavuvi wadogo kujiunga na vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) ili kurahisisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wa uvuvi wa kisasa.