Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 23Article 559210

Habari za Biashara of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wawekezaji kufaidika na fursa 30 za bomba la mafuta

Fursa 30 za uwekezaji kutolewa na mradi wa bomba la mafuta Fursa 30 za uwekezaji kutolewa na mradi wa bomba la mafuta

Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki unatarajiwa kutoa fursa za kibiashara zaidi ya 30 kwa wajasiriamali wa ndani katika uwekezaji wake kwa nchi washirika ambao ni Tanzania na Uganda.

Hatua hii imelenga katika kuhakikisha kunakuwepo na ushirikishwaji wa wazawa kwa nchi zote mbili katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo utajengwa kwa urefu wa Km 14440 kutoka katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi Mkoa wa Tanga nchini Tanzania huku gharama za mradi huo zikiwa ni takribani trilioni 8.1 za kitanzania.

Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Richard Kabonero amebainisha kuwa nchi zote mbili zimefikia makubaliano ya kutoa fursa hizo 30 za usambazaji wa mali ghafi zitakazo tumika katika ujenzi wa mradi huo huku akifafanua kuwa nafasi 17 za uzalishaji wa bidhaa zitachukuliwa na Tanzania huku Uganda wakichukua nafasi 13 za kuzalisha.

Mwisho amewataka wajasiriamali kutoka nchi zote mbili kuchangamkia fursa hiyo kubwa ya kuwekeza katika mradi huo.