Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 21Article 558805

Habari za Biashara of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Biteko atoa tathimi mpya sekta ya madini

Waziri Biteko atoa tathimi mpya sekta ya madini Waziri Biteko atoa tathimi mpya sekta ya madini

Waziri wa Madini, Dotto Biteko, amesema maonesho ya madini yanayoendelea mkoani Geita,yamesaidia kuleta mapinduzi katika sekta hiyo kwa kuboresha teknolojia ya uchimbaji wa madini.

Maonesho hayo ya nne yanawahusisha wadau wa madini, wachimbaji wa dogo na wakubwa huku yakiwa wanawakutanisha pamoja na wadau wa sekta hiyo kimataifa.

Waziri Biteko, amesema kuwa tathimini ya maonesho hayo ni kubwa hasa kwa mwaka huu kwani yamewainua wachimbaji wa madini nchini kiteknolojia kwa kuweza kujifunza mbinu mpya za uchimbaji zinazorahisha zoezi hilo pamoja na kupunguza athari za kimazingira.

"Tathmini ya maonesho ya mwaka huu inaendelea kuwa nzuri ukilinganisha na mwaka uliopita, washiriki wamekuwa wengi kuliko mwaka jana, lakini hatufurahii watu kuwa wengi, bali tunafurahi kwa kuwa kila baada ya maonesho haya lazima kuna kipya kinapatikana, uchimbaji wetu ulikuwa unatumia teknolojia duni sana lakini maonesho haya yamesaidia kuongeza utundu wa kiteknojia" Waziri Biteko.

Hata hivyo amesema kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atafungua maonesho hayo ya siku saba, na kuhitimishwa na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amehitimisha kwa kutoa wito kwa watanzania kufika katika maonesho hayo ambayo yanalenga kukuza uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa zinazopatikia hapo.