Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 07 12Article 546772

Habari za Biashara of Monday, 12 July 2021

Chanzo: dar24.com

Waziri Mkuu awasili Morocco kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu awasili Morocco kwa ziara ya kikazi Waziri Mkuu awasili Morocco kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumatatu Julai 12, 2021 amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.

Akiwasili katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.