Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 05 27Article 540067

Habari za Biashara ya

Chanzo: ippmedia.com

Waziri atamba Zanzibar kung'ara uzalishaji viungo

Waziri atamba Zanzibar kung'ara uzalishaji viungo Waziri atamba Zanzibar kung'ara uzalishaji viungo

Amesema hatua hiyo itawasaidia wakulima kunufaika zaidi na kilimo hicho na kukuza uchumi wa nchi.

Aliyasema hayo jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 202/22.

Dk. Nahoda alisema kipaumbele cha wizara katika mwaka wa fedha ni kuimarisha mazao ya viungo kwa wakulima kwa kushirikiana na asasi mbalimbali, hatua ambayo itawawezesha wakulima kupiga hatua kubwa ya kukuza kipato.

Alisema wizara imechukua hatua hiyo baada ya kubaini bei ya mazao ya viungo katika soko la dunia ni nzuri na yenye tija kwa wakulima.

Waziri huyo alisema kuwa katika miaka ya 1960, Zanzibar ilikuwa ikiongoza katika ukanda wa Afrika ya Mashariki kuzalisha mazao ya viungo na kusafirisha katika bara la Asia.

Aliyataja mazao ya viungo ambayo yatapewa kipaumbele katika mwaka wa fedha 2012/22 ni vanila, pilipili manga, pilipili hoho, uzile na mdalasini.

''Kwa mwaka wa fedha 2012/22, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kuhakikisha mazao ya viungo ya vanila, uzile, pilipili manga na pilipili hoho ambapo tumebaini kwamba bei yake ni nzuri katika soko la dunia na kuwa mkombozi kwa wakulima," alisema.

Waziri alisema wizara inaendelea na mikakati yake ya kuimarisha mazao ya nazi pamoja na karafuu ambapo jumla ya miche 500,000 ya mikarafuu itagaiwa bure kwa wakulima.

Alisema miche 500,000 ya minazi mirefu ya Kiafrika itagaiwa kwa wakulima Unguja na Pemba ili kusaidia upatikanaji wa nazi visiwani humo.

"Tumejipanga vizuri kuhakikisha Zanzibar inarudisha hadhi yake ya uzalishaji wa nazi katika Bara la Afrika na kupata mbata inayozalisha mafuta," alisema.

Dk. Nahoda aliliomba Baraza la Wawakilishi kuidhinisha Sh. bilioni 53.7 kwa kazi za kawaida na maendeleo kwa mwaka ujao wa fedha.

Kati yake, Sh. milioni 423 ni kwa ajili ya mradi wa kupambana na wadudu waharibifu wa mazao na matunda, wakiwamo nzi.

Join our Newsletter