Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 10Article 556654

Habari za Biashara of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Zaidi ya Malori 200 ya Tanzania yazuiliwa nchini Zambia

Zaidi ya Malori 200 ya Tanzania yamezuiwa nchini Zambia Zaidi ya Malori 200 ya Tanzania yamezuiwa nchini Zambia

Serikali nchini Zambia imejibu tuhuma zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kuyazuia malori 200 ya mizigo ya nchini Tanzania kuingia katika taifa hilo kwa kigezo cha kubeba mizigo haramu.

Akikanusha madai hayo, Waziri wa Kazi na usafirishaji nchini humo, Leonard Chamuhiro amesema kuwa hawajapokea taarifa yoyote kama Wizara kuhusu madai hayo kutoka kwa wamiliki wa malori hayo ya mizigo.

"Hatujapokea taarifa yoyote kutoka kwa wamiliki wa malori, na hakuna taarifa rasmi tulizozipata, labda kwasasa tufatilie tujue undani wa suala hili"amesema Waziri huyo.

Nacho chama cha Wamiliki wa magari Makubwa na Madogo ya mizigo nchini Tanzania, kupitia Mwenyekiti wao, Chuki Shaban kimesema kuwa zaidi ya magari 200 yameshikiliwa nchini Zambia kwa tuhumaza kusafirisha mizigo isiyo halali.

"Tumezuiliwa nchini Zambia licha ya kuonesha nyaraka kuwa mizigo tuliyobeba ilikwisha hakikishwa nchini Congo"amedai Mwenyiki huyo.