Uko hapa: NyumbaniBiashara2021 09 20Article 558625

Habari za Biashara of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Zanzibar yawakaribisha wawekezaji

Wawekezaji wakaribishwa kuwekeza Zanzibar Wawekezaji wakaribishwa kuwekeza Zanzibar

Waziri wanchi ofisi ya rais kazi, uchumi na uwekezaji serikali ya mapinduzi Zanzibar Mudrik Ramadhan Soranga amewalika wawekezaji kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika visiwa vya Zanzibar kwa kuwa serikali ya awamu ya nane imeweka mazingira mazuri ikiwemo sera na sheria nzuri za kuwalinda wawekezaji.

Soranga amewahakikishia wawekezaji wote kuwa katika awamu ya nane,chini ya rais dr Hussein Ally Mwinyi mambo yamebalika ambapo amekiri kuwepo changamoto kadhaa hapo awali ambazo sasa zinafanyiwa mabadiliko makubwa ili kuleta ufanisi zaidi.

Amebainisha kuwa ukiacha utalii wa fukwe na mji Mkongwe kwa upande wa bahari bado kuna mambo mengi yanayoendelea ambayo hayajaendelezwa ipasavyo.

Awali wakizungumza jijini Arusha katika hafla ya kuhamasisha wadau mbalimbali kuwekeza Zanzibar hasa katika mji mpya wa Fumba na the soul city mkurugenzi wa Homes property JERI MUYA na mkurugenzi mtendaji CPS sales Fatma Musa wamesema miji hiyo mipya inafursa nyingi za uwekezaji kama makazi na biashara.