Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2022 01 03Article 582859

Uhalifu & Adhabu of Monday, 3 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mahakama Yaridhia Ombi la Sabaya

Mahakama Yaridhia Ombi la Sabaya Mahakama Yaridhia Ombi la Sabaya

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imekubali ombi la mawakili upande wa utetezi kuondoa ushahidi wa picha za CCTV zilizokuwa ziwasilishwe na Afisa Uchunguzi wa Takukuru, Ramadhan Juma katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Juma ambeye ni Shahidi wa 13 alipaswa kutoa ushahidi wa kiuchambuzi wa picha za video zilizo rekodiwa tarehe 22 Januari, 2021, hata hivyo mawakili wa utetezi walipinga kwa kuwa shahidi huyo hana mamlaka kisheria.

Hakimu Patricia Kisinda aliiambia Mahakama Jumatatu kuwa imeridhia hoja za mawakili wa upande wa utetezi kutokana na Sheria ya Ushahidi no 17 na kwa kurejea Maamuzi ya Mahakama za juu.