Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 09 10Article 556759

Uhalifu & Adhabu of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mahakama yakubali mashahidi kufichwa kesi ya Mbowe

Mahakama imekubali Mashahidi upande wa utetezi kufichwa Mahakama imekubali Mashahidi upande wa utetezi kufichwa

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu "Mahakama ya Mafisadi" imekubaliana na maombi ya upande wa utetezi wa kuficha Mashahidi wao wanne katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake.

Awali kabla ya maamuzi hayo, Washitakiwa walisomewa makosa sita ambayo waliyakana yote na kupelekea kesi hiyo kusimama kwa muda.

Jaji Mustapha Siyani ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 15, 2021 ambapo itasikilizwa mfululizo ambapo upande wa utetezi una mashahidi 7 huku wanne wakiwa wamefichwa.