Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 09 10Article 556675

Uhalifu & Adhabu of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mbowe na wenzake wakana mashtaka yote sita

Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamekana mashtaka yao sita yanayowakabili mbele ya Jaji Mustapher Siyani.

Sasa washtakiwa hao wanasomewa hoja za awali( PH) na wakili wa Serikali, Tulimanywa Majigo.

Mbowe anashtakiwa pamoja na Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya ambao wote ni makomandoo waliofukuzwa kazi jeshini kutokana na sababu mbalimbali. Watuhumiwa wanakabiliwa na mashtaka sita, likiwamo la kukutwa na sare na vifaa vya Jeshi la Wananchi (JWTZ). Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Agosti mosi na Agosti 5 mwaka jana.