Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 09 10Article 556798

Uhalifu & Adhabu of Friday, 10 September 2021

Chanzo: Mwananchi

Miili ya watoto mapacha yapatikana ikiwa imetupwa

Miili ya watoto mapacha yatupwa Miili ya watoto mapacha yatupwa

Miili ya watoto wawili imekutwa imefungwa na kuwekwa katika mfuko imepatikana katika shamba la matunda pembeni ya Mto Sanjo kata ya Isanga mtaa wa Majahida wilaya ya Bariadi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa tukio limetokea Septemba 9, 2021 ambapo walikuta miili hiyo ikiwa katika mfuko ukiwa umeviringishwa na kanga huku ukiwa umezingirwa na siafu.

Akizungumzia tukio hilo shuhuda Melesiana Lenga amesema kuwa tukio hilo ni la kwanza katika maeneo yao na watoto waliookotwa hakuwa wamefikisha muda wa kuzaliwa.

"Kwa kuwatazama walikuwa bado hawajafikisha umri wa kuzaliwa na miili yao ilikuwa imeshambuliwa sana na siafu," amesema Melesiana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Samwel Mapalala amesema kuwa baada ya kuona miili hiyo walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

"Ilibidi kutumia moto ili kuondoa siafu katika miili ambayo ilitambaliwa na siafu kila sehemu na baadae polisi waliondoka na miili hiyo," amesema Samwel.

Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa wa Simiyu Richard Abwao amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa watoto hao walikuwa ni mapacha.

"Kwa mujibu wa daktari watoto hao wamezaliwa katika mazingira ya utoaji mimba na wanakadiriwa kuwa na kati ya miezi saba au minane kwa sababu walikuwa wametimia viungo vyote isipokuwa muda wa kuzaliwa ulikuwa haujatimia...

Walifungwa kwenye nguo kisha mfuko hivyo walikosa hewa lakini mazingira waliyokuwepo pia yalikuwa na baridi hiyo ndio sababu ya kifo chao".