Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 09 14Article 557314

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali imerejesha magari 20 yaliyoibwa nchini Kenya

Serikali imerejesha magari 20 yaliyoibwa nchini Kenya Serikali imerejesha magari 20 yaliyoibwa nchini Kenya

MKUU wa Wilaya ya Loitokitok nchini Kenya, Wesley Koech ameishukuru na kuipongeza serikali ya Tanzania kufanikisha kukamata na kurejesha magari 20 na pikipiki zilizoibwa nchini humo.

Koech amesema hayo jana mjini Loitokitok, Kenya katika kikao cha ujirani mwema kati ya wilaya hiyo na wilaya ya Rombo, Tanzania. Koech alisema serikali ya Kenya imeimarisha uhusiano wa ujirani mwema na Tanzania na wataimarisha uhusiano na wananchi wa Rombo.

Mkuu wa Wilaya ya Taveta, nchini Kenya, Joseph Maina amesema Tanzania inastahili pongezi kwa kuwasamehe na kuwachia huru maofisa polisi wa Kenya walioingia nchini wakiwa wamebeba silaha za moto. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamisi Maigwa amesema serikali ya Tanzania imejipanga kuondoa kero na vikwazo vinavyoathiri ujirani mwema kati ya Rombo na Loitokitok.