Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 11 23Article 573739

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Shahidi aeleza walivyowakamata watuhumiwa kesi ya kina Mbowe

Shahidi aeleza walivyowakamata watuhumiwa wa ugaidi kesi ya kina Mbowe Shahidi aeleza walivyowakamata watuhumiwa wa ugaidi kesi ya kina Mbowe

Shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo ameieleza mahakama alivyoshiriki katika kuwakamata na kuwasafirisha hadi Dar es Salaam watuhumiwa wawili katika kesi hiyo.

Akitoa ushahidi wake leo Jumanne Novemba 23, 2021 Askari mpelelezi DS Goodluck amesema alimfahamu mtuhumiwa wa tatu baada ya watuhumiwa wenzake kumtaja kwa jina la Kakobe au Moses Lijenje.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.

Kesi hiyo inasikikizwa na Jaji Joachim Tiganga.

Jaji: Shahidi jina lako

Shahidi: Namba H 4347, Detective Sajenti Goodluck (32), kabila mchaga, dini yangu Mkristu.

Ni skari Polisi na nimeajiriwa na jeshi la Polisi tangu mwaka 2013.

Ni mkazi wa Arusha tangu mwaka 2014. Kituo changu cha kazi Arusha, Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.

Agosti 3, 2021 ndio nimepandishwa cheo na kuwa Sajenti.

Shahidi: Mwaka 2020 nilikuwa Constable. Kwa Sasa nipo Idara ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai, kwa muda wa miaka mitatu. Majukumu yake mengine ni Kupeleleza, kukamata wahalifu, kusimamia Askari waliochini yangu, kukusanya vielelezo na kutekeleza majukumu nitakayopangiwa.

Shahidi: Agosti 4, 2020, nilikuwa ofisi kwangu katika kituo cha Polisi Arusha,

Shahidi: Majira ya jioni, Afande Mahita alinipigia simu na kuniita ofisi kwake.

Nilipofika ofisi kwake, aliniita niende ofisi kwake nikiwa na Afande Francisi.

Kipindi hicho Mahita alikuwa Msaidizi wangu Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha.

Shahidi: Kwa Kipindi hicho RCO alikuwa Afande Kingai

Shahidi: Tulipofika ofisini kwake, alituambia tujiandae kwa safari.

Shahidi: Baada ya kuambiwa hivyo tuliondoka na kwenda kuchukua silaha.

Shahidi: Baada ya kuchukua silaha, tulipanda kaitumia gari la afande RCO, Mimi, Mahita, Francisi, Dereva na Kingai

Shahidi: Kingai alituambia tunaelekea kituo Cha Polisi Usariva ambapo alisema tumpigia afande Jumanne ambaye alikuwa OCCID.

Shahidi: Tulipofika kituo Cha Polisi Usariva, Afande Kingai alitupa brief ya kitu tunachoenda kufanya

Shahidi: Katika brief hiyo, Kingai alisema kuna watu wanaenda kuwakamata kuna kikundi cha watu kimekula njama ya kufanya vitendo vya kigaidi katika maeneo ya Arusha, Dar, Mbeya na Mwanza

Shahidi: Katika briefing, Kingai alitueleza kuwa katika kikundi hicho, kuna watu ambao wapo Moshi, hivyo tunatakiwa kwenda kuwakamata.

Shahidi: Agosti 5, 2020 tuliekekea Moshi kwa ajili ya ukamataji na tulifika saa 7:00 mchana eneo la Rau.

Shahidi: Tulikuwa tunaenda kuwakamata watu watatu, lakini tulifanikiwa kuwakamata watu wawili ambao Ni Mohamed Ling'wenya na Adamu Kasekwa

Wakili wa Serikali, Hilla: Je watu uliowakamata Moshi wapo hapa mahakamani?

Shahidi: Wapo hapa mahakama.

(Shahidi anasogea katika kizimba cha washtakiwa na kuwataja majina)

Shahidi: Huyu ni Mohamed Ling’wenya wa pili kutoka kushoto Adam kasekwa.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi amewatambua washtakiwa mahakamani.

Shahidi: Baada ya kuwakamata tuliekekea Kituo Kikuu cha Polisi Moshi.

Shahidi: Baada ya kufika kituoni, Jumanne na Mahita walishuka chini, mimi, Francisi na dereva tulibaki ndani ya gari.

Shahidi: Lengo la kubaki katika gari ilikuwa ni kuwalinda washtaki hao kwani bado tulikuwa na safari ya kwenda kumtafuta mtuhumiwa wa tatu katika maeneo mbalimbali.

Shahidi: Mtuhumiwa wa tatu nilimfahamu baada ya watuhumiwa kumtaja kwa jina la Kakobe au Moses

Shahidi: Baada ya kutoka kituo cha Polisi tulienda kumtafuta Moses maeneo ya Rau madukani. Pia tulienda maeneo ya KCMC, Majengo, Pasua, Aishi na Boma.

Shahidi: Aishi ipo Machame na Boma ipo wilaya ya Hai.

Shahidi: Utafutaji wa Moses uliendelea hadi majira ya saa tano usiku na hatukufanikiwa kumkamata.

Shahidi: Baada ya kushindwa kumkamata saa tano tulirudi Kituo cha Polisi Moshi na Kingai alielekeza watuhumiwa hao wawekwe lockup (mahabusu).

Shahidi: Baada ya Maelezo hayo, wote tulishuka katika gari na Afande Jumanne na Mahita waliwakambidhi watuhumiwa kaunta.

Shahidi: Alfajiri ya Agosti 6, 2020 tulienda kituo cha Polisi Moshi na kuwachukua watuhumiwa hadi katika kituo Kikuu cha mabasi cha Moshi.

Shahidi: Watuhumi walisema huenda Moses anaweza kusafiri kwa basi, hivyo tulienda.

Shahidi: Tulizunguka eneo la stendi ya mabasi lakini hakufanikiwa kumkamata.

Shahidi: Baada ya kushindwa kufanikiwa kumkamata katika stendi hiyo, tulipita katika maeneo ambayo jana yake tulipita.

Shahidi: Maeneo yote tuliyopita, tulikuwa tunapelekwa na watuhumiwa wenyewe.Tofauti na maeneo tuliyopita jana yake, maeneo mengine tuliyopita ni Arusha.

Shahidi: Tulienda Arusha kwa sababu, mmoja wa watuhumiwa alisema Moses anadada yake ambaye anaishi Arusha. Matokeo ya ufutaliaji eneo la Arusha, hatukufanikiwa kumpata Moses. Baada ya kushindwa kumkamata Moses, tulirudi Moshi.

Shahidi: Baada ya kufika Moshi, Kingai alituambia kuwa amepewa maelekezo kuwa watuhumiwa tuwapeleke Dar es Salaam.

Shahidi: Safari ya kwenda Dar es Salaam, ilifanyika Agost 6, 2020 saa moja jioni.

Shahidi: Nakumbuka Dar es Salaam tulifika Agost 7, 2020 majira ya Alfajiri. Tulipofika tuliekekea kituo Kikuu cha Polisi Central Dsm.

Shahidi: Tulipofika Central Dsm, tuliekekea sehemu ya mapokezi ( Charger Room- CRO) kwa lengo la kuwakabidhi watuhimiwa ili wawekwe lockup.

Shahidi: Hapo CRO, Kingai na Jumanne waliwakabidhi watuhumiwa.

Shahidi: Baada ya kuwakabidhi watuhimiwa hapo CRO, Kingai alitoa maelekezo ya short break (Kunawa uso) halafu turudi kituoni.Tulifanya hivyo na tulirudi kituoni majira ya saa moja asubuhi.

Shahidi: Tulivyorudi sa moja, Kingai alitoa maelekezo nikakabidhi vielelezo.

Shahidi: Kingai alituambia amepata taarifa kuna wahalifu hivyo alituelekeza tuendelee kufanya Upelelezi ili wao(Kingai na Jumanne) wabaki pale kituo kuandika maelezo ya washtakiwa.

Shahidi: Wakati wote kuanzia Agosti 4 Hadi kukabidhiwa kituoni, watuhumiwa walikuwa chini ya ulinzi wa Afande Mahita pamoja na mimi.

Shahidi: Wakati wote tunazunguka , watuhumiwa walikuwa katika hali nzuri, hakukuwa na malalamiko yoyote. Baada ya Agosti 7, 2020 kufika Dsm Central, mimi na mwenzangu tulifuatilia taaarifa tulizopewa na Kingai.

Shahidi: Agosti 8, 2020 ndio siku niliyowaona kwa mara nyingine baada Kingai kunielekeza niwahamishe watuhumiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Central na kuwapekea Kituo cha Polisi Mbweni. Na watuhumiwa hao walikuwa katika hali nzuri.

Shahidi: Tuliwapitia Central Dsm majira ya saa 4 asubuhi, na walipofikishwa Kituo cha Mbweni, watuhumi walikabidhiwa na kuwekwa mahabusu.

Shahidi: Mazingira ya ukamataji siku Ile yalikuwa ni salama na hakukuwa na purukushani.

Shahidi: Eneo la Rau ni eneo la wazi na watu wanafanya biashara zao. Hiyo Agosti 5, 2020 tukiwa eneo la Boma tunamtafuta mshtakiwa wa tatu, afande Kingai alishuka katika gari na muda mfupi alikuja na mtu akiwa amebeba chakula ambacho ni ndizi, nyama na vinywaji.

Shahidi: Tukiwa tunarudi Dsm, tulipofika njia Panda ya Himo gari ilipata hitilafu ya umeme na hapo afande Kingai alinunua chakula tukala wakati tukisubri gari kutoka kwa RPC wa Kilimanjaro, lije lituchukuue.

Shahidi: Siku hiyo tulikula chakula kwa pamoja na watuhumiwa.

Wakili wa Serikali, Hilla: Shahidi yapo mahalalamiko hapa mahakamani kwamba baada ya kuwakamata watuhumiwa kule Moshi siku Ile ya Agosti 5, 2020 , baada ya kuwapeleka Kituo cha Polisi Moshi, wanasema wewe uliwatesa ? Je wewe unaeleza nini Mahakama.

Shahidi: Hapana hawakuteswa kwa sababu tulipofika Kituo cha Polisi Moshi, mimi sikushuka kituoni pale.

Shahidi: Pia tulivyofika Moshi tulifika Dsm Kituo Kikuu cha Polisi na kuwakabidhi.

Shahidi: Na kulikuwa hakuna mazingira yoyote ya kuwatesa watuhumiwa.

Wakili wa Serikali Hilla: Shahidi yapo pia malalamiko kuwa washtakiwa hawakufikishwa kituo Kikuu cha Polisi Central na Agosti 9, 2020 wewe na Afande Jumanne mkiwa kituo cha Polisi Mbweni , wewe ukiwa na bastola ulimtishia mshtakiwa Ling'wenya kuwa asiposaini maelezo yake, mateso ya Moshi yatajirudia rudi.

Shahidi: Watuhumiwa hawajateswa na hakuna sehemu yoyote waliyoteswa. Pia watuhumiwa hao walifikishwa kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.Kwa hiyo hakuna mazingira yoyote ambapo watuhumiwa waliteswa.

Shahidi: Hata hiyo Agost 8, 2020 mimi na wenzangu tulivyowafikisha watuhumiwa hao wawili kituo cha Polisi Mbweni, sisi tuliwaacha pale na kuendelea na upelelezi.

Shahidi: Pia Agosti 9, 2020 mimi na wenzangu tuliendelea kuwatafuta washtakiwa wengine ambapo tulifanikiwa kumkamata Halfan Bwire Hassani.

Wakili wa Serikali, Hilla: Vipi suala la kumlazimisha Lingw'enya kusaini maelezo yake na kama hata fanya hivyo, mateso ya Moshi yatajirudia rudia?

Shahidi: Hakuna sehemu aliyolazimishwa kusaini kwani kazi ya kuwapeleka Kituo cha Polisi Mbweni ilifanywa na mimi afande Jumanne na Ispekta Swilla na tulivyowafikisha hapo, mimi nilindoka.