Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2021 09 11Article 556822

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 11 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Watatu Wakamatwa na Shehena ya Risasi, Silaha za Kivita

Watatu Wakamatwa na Shehena ya Risasi, Silaha za Kivita Watatu Wakamatwa na Shehena ya Risasi, Silaha za Kivita

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na risasi 1,493 za silaha za kivita wilayani Nkasi.

Tukio hilo limetokea juzi Jumatano, Septemba 8, 2021, majira ya saa 7:45 mchana katika Kijiji na Kata ya Kotongwe, Tarafa ya Kirando.

Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani humo imeeleza kuwa mbali na risasi hizo, jeshi hilo pia liliwakuta watuhumiwa hao wakiwa na silaha za kivita aina ya AK47 na SAR Kinyume vha sheria.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa, wavuvi 7 walizikuta risasi hizo zikiwa mapangoni wakidhani ni madini ya dhahabu na waliwapatia watuhumiwa nao wakazinunua.

Watuhumiwa hao walikamatwa na walipohojiwa walishindwa kueleza walikuwa wanazipeleka wapi japo walizitambua kuwa ni risasi za moto.

Polisi imesema upelelezi wa kina zaidi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.