Uko hapa: NyumbaniHabariUhalifu & Adhabu2022 01 14Article 585820

Uhalifu & Adhabu of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Watatu mbaroni wizi wa scania Pwani

Watatu mbaroni wizi wa scania Pwani Watatu mbaroni wizi wa scania Pwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za wizi wa gari (Scania) , gari hilo limekamatwa January 13,2022 katika Kijiji cha Pingo Wilayani Chalinze wakati likitokea Dar es salaam kwenda Mwanza.

Waliokamatwa ni Hemedi Rajabu (32) na Lusandi Mauya (49) wote ni Madereva pamoja na Deosdedit Kimario (32) ambaye alikuwa Kondakta wa gari hilo ambalo lilibeba mzigo wenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 200 zikiwemo tani 30 za nondo na magodoro ya size mbalimbali 341.

"Mbinu iliyotumika ni kubadili namba za usajili halisi za gari namba T 317 DWL kwenye horse na T 804 BMF kwenye trailler na kuweka namba bandia T 364 DDK kwenye horse na T 467 DTL kwenye trailler" ——— RPC Pwani