Uko hapa: NyumbaniInfosDiaspora2020 09 25Article 510241

Diasporian News of Friday, 25 September 2020

Chanzo: Zanzibar 24

DKT SHEIN ASEMA THABIT KOMBO ALIKUWA ANAMCHANGO MKUBWA NDANI YA ZANZIBAR

DKT SHEIN ASEMA THABIT KOMBO ALIKUWA ANAMCHANGO MKUBWA NDANI YA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa lengo la kuliita jengo hilo jina la THABIT KOMBO BULDING ni kuziunga mkono jitihada zake na kuenzi mchango wake alioutoa kwa wazanzibar.

Hayo ameyasema wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Jengo la Thabit Kombo Building (Kisonge) ambapo sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na yeye Mwenyewe Mhe Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni rais wa Zanzibar.

“Kawaunganisha wazanzibar wa Unguja na Pemba kwa kuviunganisha Vyama viwili na kuwa chama kimoja chenye nguvu, hatuwezi kufanya jambo lolote la chama au kwa Zanzibar bila kumpa heshma Sheikh Abeid Amani Karume na Sheikh Thabit Kombo na hio ndio sababu ya Serikali kuliita Jengo hili Jina lake”

Pia Dkt Shein amesema “Marehem Thabit Kombo hakufanya kazi za Chama pekee alifanya kazi za Serikali , Thabiti Kombo ananafasi maalumu katika Zanzibar na anahaiba maalumu ndani ya Chama” amesema Dkt. Shein

Nae Waziri wa Fedha na mipango Zanzibar Balozi Mohd Ramia amesema ” CCM ni chama chenye kuaminika na ZSSF kuingia Ubia, kuingia Mashirikiano na chama hamkokosea hata kidogo , mumeingia mkataba na taasisi yenye kuaminika, ccm inafanya jambo lenye manufaa kwa wananchi wake “

Jengo hilo la Thabit Kombo Building linaghorofa 5, ardhi inasehemu ya maegesho ya gari pamoja na maegesho ya vyombo vya maringi mawili, na mnamaduka 48 ya biashara na yatakodishwa , na ghorofa nyengine kutakua na ofisi kwajili ya kukodishwa na ghorofa nyengine itakua kwaajili ya Ofisi ya Maskani Kaka ya Kisonge pamoja na ukumbi wa Mikutano.

Ujenzi huo umekamilika kwa ahadi ya rais Dk. Shein ambapo aliwaahidi wanamaskani hao kuwajengea maskani mpya baada ya kuunguzwa moto maskani hio mnamo mwaka 2012 Octoba 18 iliunguzwa moto na watu wasiopenda maendeleo.

Chama cha Mapinduzi CCM kimeshirkiana na ZSSF, kupitia maskani kaka ya Muembe kisonge ambao ndio wamiliki halali wa eneo hilo.

STORY NA RUWAIDA SALEH NA HAMID KHAMIS.

Join our Newsletter