Uko hapa: NyumbaniHabariDiaspora2021 06 10Article 541969

Diasporian News of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Dk. Mwinyi akunwa na mkakati Small Simba

Dk. Mwinyi akunwa na mkakati Small Simba Dk. Mwinyi akunwa na mkakati Small Simba

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa Klabu ya Small Simba, ambayo siku za nyuma iliwika katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya Zanzibar.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi, alisema moja kati ya ahadi zake katika kampeni za uchaguzi mkuu, ilikuwa ni kurejesha hadhi ya michezo kama au zaidi ya ilivyokuwa katika uongozi wa serikali ya za awamu zilizopita, jambo ambalo litafanywa na wadau wa michezo na serikali jukumu lake ni kuweka mazingira mazuri.

Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba mafanikio katika sekta ya michezo, hayawezi kupatikana iwapo hakutowekwa mazingira mazuri katika sekta hiyo, hivyo Serikali ya Awamu ya Nane, itaendelea kushirikiana na wadau wote wenye azma ya kuiimarisha sekta ya michezo ili kuhakikisha inaimarika.

Alitoa pongezi kwa uongozi huo kutokana na mawazo yao ambayo yanaendana na yale ya serikali yake kuanzia chini kwa kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana huko Fuoni Kibondeni jambo ambalo ni jema na aliliunga mkono huku akisisitiza kwamba nchi zote zilizofanikiwa katika soka duniani zimeanzia na vituo vya mafunzo na kuibua vipaji vya vijana wakiwa wadogo.

Alisema kwa vile tayari timu hiyo imeshapatiwa eneo la kudumu la kufanyia shughuli zao, ni jambo jema ambapo hatua inayofuata ni kuhakikisha linakuwa na miundombinu inayotakiwa hasa ikizingatiwa kwamba tayari wameshalifanyia upembuzi yakinifu.

Rais Dk. Mwinyi aliunga mkono maelezo ya uongozi huo kwamba michezo ni biashara na si burudani peke yake hivyo, ni vema klabu zote zikaendeshwa kibiashara hatua ambayo itasaidia kutoa ajira pamoja na kuongeza ari ya vijana kujinga katika michezo.

Join our Newsletter